10 Oktoba 2025 - 13:59
Taarifa ya Ubalozi wa Iran kuhusu Upotoshaji wa Vyombo vya Habari vya Kiingereza

Ubalozi wa Iran nchini Uingereza umejibu upotoshaji wa vyombo vya habari vya Kiingereza kuhusu wakimbizi wa Afghanistan walioko Iran, na umepinga madai ya uongo yaliyotolewa na vyombo hivyo vya habari vya Kiingereza kwamba kuna uwezekano wa kufukuzwa kwa mamia ya maelfu ya wakimbizi wa Afghanistan kwenda katika nchi jirani.

Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Ahlul-Bayt (a.s) -ABNA- Ayoub Heydari, msemaji wa ubalozi wa nchi yetu nchini Uingereza, amejibu hatua ya vyombo vya habari vya Kiingereza katika miezi ya hivi karibuni ya kuchapisha habari na ripoti nyingi hasi kuhusu mwenendo wa Iran kwa wakimbizi wa Afghanistan na madai ya kuwafukuza, ikiwemo gazeti la The Guardian ambalo lilichapisha taarifa ya uongo kuhusu kufukuzwa kwa wakimbizi wasio halali kutoka Iran kwenda katika nchi jirani.

Ayoub Heydari katika barua yake kwa gazeti la The Guardian ameandika kuwa: “Kwa zaidi ya miongo minne iliyopita, Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, licha ya mashinikizo makubwa ya kiuchumi yanayotokana na vikwazo vya upande mmoja na ukosefu wa karibu kabisa wa misaada ya kutosha ya kimataifa, imekuwa mwenyeji wa mamilioni ya wakimbizi wa Kiafghanistan na imekuwa ikiwapatia huduma za kibinadamu za elimu na afya.”

Katika muendelezo wa barua hiyo imeelezwa kuwa: “Wakati Iran ikiendelea kubeba jukumu hili zito kwa kiasi kikubwa peke yake, msaada wa kimataifa kwa ajili ya uenyeji na ujumuishaji wa wakimbizi nchini humo umesalia kuwa mdogo mno ukilinganishwa na kiwango cha mahitaji halisi.”

Msemaji wa ubalozi wa Iran katika sehemu nyingine ya barua hiyo akilielekeza kwa The Guardian ameandika kuwa: “Ripoti yenu inadai kwamba Iran inazingatia kuwaruhusu idadi kubwa ya wakimbizi waende katika nchi jirani, ilhali hakuna sera au uamuzi kama huo uliotangazwa na mamlaka husika za Iran. Sera ya Iran kuhusu wakimbizi imejengwa daima juu ya misingi ya kibinadamu, kuheshimu hadhi ya mwanadamu, na kushirikiana na taasisi za kimataifa zinazohusika.”

Mwisho wa barua hiyo unasema:

“Kuchapisha taarifa ambazo hazijathibitishwa au zilizo pungufu kuna hatari ya kupotosha ukweli ulioko eneo husika na kupoteza uelewa sahihi wa umma.”

Tags

Your Comment

You are replying to: .
captcha